Jumanne ya March 14, 2017 kupitia #Clouds360 ya Clouds TV, staa wa BongoflevaNaseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz amefanya interview na kueleza mambo mengi kuhusu muziki wa Tanzania, serikali kusaidia sanaa, Rais kuweka mkono wake kwenye muziki, wasanii kulipa kodi, kutangaza utalii na kipi kinaendelea kati yake na staa mwenzake Alikiba.
Nimekukusanyia hapa mambo 15 ameyaongea leo Diamond Platnumz.
Naomba serikali iwasaidie vijana wa vibanda vya chipsi pamoja na bodaboda ishu ya muda wa saa sita wapewe ulinzi#DiamondPlatnumz #Clouds360
Tumeshirikiana na Joseph Kusaga kuaanda product ya Chibu Perfume, tutazindua bidhaa hii fahari ya Tanzania #DiamondPlatnumz#Clouds360
Hili suala la Serengeti Boys ni jukumu letu kulibeba kama Taifa tuunganishe nguvu ushindi wetu ushindi wao #DiamondPlatnumz#Clouds360
Nilikutana na #Alikiba Nairobi tukazungumza, maneno yanasemwa na watu wa katikati baadhi ya media zinachochea tu#DiamondPlatnumz #Clouds360
Tulilipa Kodi ya TRA milioni 35 ni uthubutu tunaweza kulipa kodi nyingi, serikali inabidi itulinde kwenye sanaa #DiamondPlatnumz#Clouds360
Watu walizungumza vibaya mimi kupewa BenderΓ ilisaidia sana kulitangaza taifa letu, nilimuomba Nape samahani#DiamondPlatnumz #Clouds360
Kipindi tunamuaga Rais Kikwete nilipata nafasi ya kuzungumza na Rais Magufuli nilimuomba tupate ukumbi wa kisasa#DiamondPlatnumz #Clouds360
Mimi ni kielelezo ndani na nje ya nchi watu wengi wameifahamu tanzania kupitia sanaa yetu lazima tujijenge #DiamondPlatnumz#Clouds360
Tangu mwezi wa 7 mpaka sasa sijapokea mauzo yangu nimeyasusa, kinachofuata itakuwa ni hatua za kimahakama #DiamondPlatnumz#Clouds360
Makonda ni mlezi wa WCB kila mwanadamu ana mapungufu yake tuangalie pia mazuri, ameonesha uthubutu kwenye kazi#DiamondPlatnumz #Clouds360
Msanii akihusishwa kwenye sakata la dawa za kulevya ni kuharibu brand, Serikali itumie busara kuzilinda na kesi. #DiamondPlatnumz#Clouds360
Nilishawahi kwenda TANAPA kuomba niwe balozi wa utalii nitangaze nchi yangu lakini walitaka nijitolee bure tu. #DiamondPlatnumz#Clouds360
Tumeanzisha mtandao wetu wa kuuza na kusambaza nyimbo za wasanii online tumeongea na mashabiki watuunge mkono#DiamondPlatnumz #Clouds360
Watu wanashangaa mimi kutangaza vivutio vya Afrika Kusini sio kwamba nimekosa uzalendo, wameniona kupitia sanaa #DiamondPlatnumz #Clouds360
DOWLOAD APP YETU YA WCB DAILY HAPA CHINI
0 Response to "Mambo 15 aliyoyaongea Diamond Platnumz leo kwenye kipindi cha Clouds360 cha Cloudsfm"
Post a Comment